Mwandishi: Ben Mtobwa
Synopsis:
Inspekta Kombora anaitwa katika hoteli moja jijini Dar es Salaam ambapo anaonyeshwa mwili wa msichana aliyeuawa kikatili kupita kiasi. Ngozi na nyama ya uso wake mzima na sehemu ya shingo zimeliwa na aina fulani ya sumu na kufanya sura yake ibakie kuwa fuvu la kutisha. Katika kinywa cha fuvu hilo, uliwekwa ujumbe kwa maandishi uliosomeka: Tunamtaka Joram Kiango.
Salamu zinamfikia Joram kwa namna nyingine. zikifuatiwa na patashika nzito, roho mkononi, huku watu wengi walio na wasio na hatia wakipoteza roho zao. Lakini ni roho ya Joram Kiango iliyohitajika, kwa udi na uvumba. Naye, akijua kuwa anapambana na mbogo waliojeruhiwa, alichukua tahadhari zote kutopoteza uhai mithili ya paka. Hata roho yake pia inabadilika na kuwa Roho ya Paka.
Description
SKU: 9789987083848
Publisher: Mkuki na Nyota