Mwandishi: E. A. Musiba
Synopsis:
Mauaji ya kikatili yanafanyika karibu na mji wa Uitenhage nchini Afrika Kusini, siku ya kuwakumbuka wazalendo waliouawa mjini Sharpeville mwaka 1960. Makaburu wanajawa na hofu na wanatilia shaka kuwa ni njama za kikundi cha watu weusi kutaka kupindua serikali yao ya kibaguzi.
Uongozi wa makaburu wa Afrika Kusini wakiongozwa na mkurugenzi wa shirika la ujasusi, kamanda wa jeshi la Kulfut na mkuu wa magaidi wasaliti wa UNITA wanakutana ili kukabili juhudi za ukombozi wa Afrika Kusini kwa kupanga wimbi la mauaji.
Mkutano wa wapigania uhuru wa Afrika Kusini unafanyika Arusha, nchini Tanzania. Jambo hili linawatia hofu makaburu, hivyo basi, mikakati kabambe inafanywa na serikali yao ili kuusambaratisha mkutano huo.
Umoja wa Wapigania Uhuru nao unaandaa kikundi makini kabisa ili kupambana nao na kuulinda mkutano huu muhimu.
Mpelelezi nguli wa Afrika, Willy Gamba, hakosi panapokuwa na mapambano kati ya upande wenye haki, na ule wa dhuluma. Kwa kushirikiana na wapelelezi mahiri kutoka nchi za kusini mwa Afrika, wanakabiliana na makaburu hao na vikundi vya kigaidi vinavyoshirikiana nao.
Hekaheka zinatokea Arusha, hofu inatanda kote! mwindaji awa mwindwaji…
Description
ISBN | 9789987083275 |
Pages | 162 |
Dimensions | 198 x 129mm |
Published | 2018 |
Publisher | Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania |
Format | Paperback |