Author: UONGOZI Institute & Sokoine University of Agriculture (SUA)
Synopsis:
Ni majira ya alasiri, kiasi cha saa tisa hivi, siku ya Alhamisi, Aprili 12, 1984. Ghafla Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD – sasa TBC), redio ya taifa na pekee Tanzania Bara wakati ule, inakatisha matangazo ya vipindi vyake vya kawaida, na Wimbo wa Taifa, Mungu Ibariki Tanzania, unapigwa. Wimbo unamalizika, na sauti iliyozoeleka sana kwa wananchi, lakini zamu hi ikiwa na tulivu mkubwa, inaanza kuelezea taratibu, polepole, tena kwa kituo na majonzi makubwa, ikisema: “Ndugu wananchi, leo mnamo saa saba mchana, ndugu yetu na kijana wetu, Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipokuwa anarudi Dar es Salaam kutoka Dodoma, gari yake ilipata ajali. Amefariki dunia.” Ghafla, siku iliyokuwa ya kawaida kabisa, watu wakiendelea na Maisha yao na kazi zao na matani yao, ukiwamo utani wa kandanda wa Simba na Yanga, ikawa siku ya msiba mkubwa. Kitabu hiki kinakusafirisha hadi kwenye eneo la ajali iliyokatisha uhai wa kiongozi huyu shupavu, na kinatoa maelezo ya mashuhuda wa ajali hiyo na hata uvumi uliosambaa baada ya kifo chake. Kwa upana wake, kitabu hiki kitakufahamisha maisha halisi ya Hayati Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa tatu wa Tanzania; alikotokea, familia yake na uongozi wake.
Description
SKU: 978-9987-449-81-1
Dimensions | 150 × 130 mm |
---|