Mwandishi: E. A. Musiba
Synopsis:
Ni nani hasa anayewaua viongozi wa wapigania uhuru? Kwa nini wengi wa viongozi hawa wameuawa jijini Kinshasa kuliko mahali pengine popote Afrika?
Ili kukomesha vitendo hivi vya kijahili, Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) inakata shauri kuwasaka wauwaji hawa na kuwafagilia mbali. Willy Gamba, mpelelezi maarufu wa Afrika, anachaguliwa kuongoza kikosi cha wapelelezi wa Kiafrika kuwasaka.
Kinshasa, jiji linalosifika kwa starehe zake linageuka uwanja wa mapambano kati ya vijana wapiganaji shupavu wakiongozwa na Willy Gamba, na wapinga mapinduzi wakiongozwa na Kaburu Pierre Simonard.
Willy pamoja na kikosi chake wanalivamia jiji la Kinshasa kuhakikisha wanakomesha mauaji hayo. Ndipo patashika ambalo halijawahi kutokea barani Afrika linapoanza na kuliwasha moto jiji hili…
Description
ISBN | 9789987083183 |
Pages | 234 |
Dimensions | 198 x 129mm |
Published | 2018 |
Publisher | Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania |
Format | Paperback |